Na Hadji Helper,
Walipofika nyumbani wakagundua kuwa mengi ya mayai yale yalikuwa yameharibika. Wakarudi mpaka sokoni na kumkuta CHACHA MWIZI akiendelea na uchuuzi wake.
Wakamlalamikia kuhusu bidhaa alizowauzia naye akakubali KUWABADILISHIA na kuwapa MENGINE. Cha kustaajabisha kufika tena nyumbani wakagundua kuwa hata yale waliyopewa yalikuwa yameharibika.
BABA MKWE kwa hekima kubwa akamshauri KILONZO kutonunua Mayai tena toka kwa CHACHA MWIZI kwani inaonekana hana bidhaa nzuri yamkini.
Kama ikibidi basi ajaribu kubadilisha mchuuzi na labda anunue toka kwa mzee CHAMWEMA au hata kwa NASSORO au ikibidi kwa CHAFU.
Hadithi hii inatufundisha mengi sana WATANZANIA, tumefikia wakati sasa WANASIASA wanatuona kama MAZUZU kwenye nchi yetu wenyewe. Ni wakati wa kuamka, kupigania chetu na kudai haki zetu. Bilioni 550 iliyopotea waeleze iko wapi na sio kutubadilishia Mayai kila siku.
Mayai haya yanatakiwa yapelekwe mahakamani na kama siyo yote, baadhi yafungwe na kurejesha mali ya wizi.
Tushajua pakacha zima limeoza.
Inasikitisha na inahudhunisha na ikumbukwe SIASA ni mchezo mchafu sana na hiki utakachopigania leo ni kwa ajili ya WATOTO au WAJUKUU zako. Ni wakati wa mabadiliko ama CHACHA MWIZI abadili mfumo mzima wa upatikanaji wa bidhaa zake au WATU hatununui bidhaa zake kabisaaaa!!!